USHUHUDA WA KIBAIGWA
Baada ya kumaliza huduma zanzimbar nilisikia sauti ya
Bwana ikiniambia kwenda Dodoma kwa wiki
mbili mbele,nikampigia mchangaji GIDION mda huohuo,Akakubali na kutukaribisha
kwa moyo wote,tukamsihi Bwana kutupa kibali cha kwenda na ndugu yangu wa
thamani CHARLES,siku ya kwenda kulikuwa na vikwazo vingi sana hadi ndugu yangu
akakwama moja kwa moja.
Bwana akanipa kibali
cha kwenda na nikafika salama siku ya ijumaa jioni tarehe 23/8/2013,kesho yake
tukaanza mkutano wetu,ulikuwa ni mkutano ambao Bwana mwenyewe alikuwa kazini
kwani nilimuona kwa dhahiri sana,
Mchungaji mmoja wa
kipentekoste alikuja mkutanoni na akasema nimekuja kujifunza na uchungaji
wangu nimeacha pale nje,alikuja pamoja na baadhi ya washirika wake, usingeweza kujua kuwa kulikuwa na wageni bali
wote tulionekana ni familia ya
BRANHAM,kwa NENO ambalo Roho alikuwa
akileta pale kuanzia kwangu kama mhudumu nilipewa palepale nami nikakituma kama lilivyo kwenye
kusanyiko.
Palikuwa na dada
mmoja jina lake akiitwa Dada Mariam Chilongani (tazama picha)alikuja kwenye mkutano baada ya
ndugu Peter ambaye
alikuwa mchungaji wa kipentekoste pia amebatizwa yeye na mke wake miezi michache iliyopita,alimwalika
kuja kwenye mkutano, lakini kuna mama mmoja mke wa mchungaji wa kanisa la kipentekoste,alimwambia kuwa hiyo
imani wanaabudu vitu vya ajabu wana imani ya ajabu sana usiende kamwe,… Huku
kukiwa na nguvu ya ajabu ikimwambia nenda.
Hatimaye
akafanikiwa kuja kwenye mkutano huku
akiwa amejaa wasiwasi mkubwa kwamba hawa watu
wanaamini ujinga,akiwa kwenye ibada anasema nilipoanza kuhubiri alikuwa na dharau kubwa kuhusu,mimi yaani
aliona kama ni kupoteza mda tu.
Ghafra anasema”nilipokuwa naangalia nikaona
muko wawili, na huyu wa pili anafunua KITABU na wewe unasoma na popote
unapozunguka mimbarani upo pamoja naye,nikawa sielewi ni kweli naona mtu
mwingine pale au? na ameenda saa ngapi mbona wote tumekaa? na wenzangu wanaona
kama ninavyomuona?nikafikisha macho,bado naona muko wawili,na huyu wa pili
amevaa kama wewe,mmefanana sana yaani kama naona taswira yako kwenye kioo. ila
ameinama sikumuona sura yake lakini mlifanana,(THIOPHAN) na kila
Ulichosema alipokuonyesha pa kusoma
kilichoma mimi kile ninaishi katika
maisha yangu niakaanza kuogopa maana naliona akikufuata kisha akatoweka ghafla
huku nikioana kila kitu.”
“Nikajua hapa huyu ni Mungu kabisa,endelea
kuhubiri injili uko na Roho mtakatifu
kabisa popote unapokwenda nimemuona kwa macho yangu na anakutumia kweli usirudi
nyuma songa mbele,na mimi sijabaki nilivyokuwa
najisikia amani sana moyoni kwani Mungu amenipa uhakika tofauti na
nilivyoambiwa,naomba maombi sana ili Bwana anibadilishe nifanane naye,alisema
dada …….”
Namshukuru sana Bwana kwani dada alishuhudia
kusanyiko la hapo na kila mmoja alibakia nashangaa na kuogopa.
Baada ya siku kama tatu hivi huyu dada aliporudi
kijijini kwake akawa anamshuhudia mama mmoja mambo aliyiyaona kwenye mkutano na
kile sisi tunaamini, YULE MAMA AKASEMA
WAKO WAPI HAO WATU NIMEKUWA NAWATAFUTA MIAKA MINGI SANA TANGU NILIPOSIKIA TOKA
KWA MHUBIRI MMOJA MOSES KULOLA MIAKA HIYO AKISEMA KUNA MJUMBE ALIYE LETA NENO LA WAKATI WETU,ANAITWA
BRANHAM,NILIPENDEZWA SANA NA HUO UJUMBE NIKATAMANI KUUJUA ZAIDI,..NIAMBIE WAKO
WAPI NAENDA KUBATIZWA TANGU LEO MIMI SI MPENTEKOSTE TENA.
Kijiji kizima kikawa kimesikia kile dada
aliona na mke wa mchungaji alikokuwa dada anasali alikuja kumfuata na kumwambia
imani gania hiyo? Ambayo hawaamini katika kunena kwa lugha,…akamwambia
nimeshawishika na sasa ninahusika, ninamfuata nabii BRANHAM ambaye nina uhakika
yuko mbinguni na siwezi kufuata wale ambao sina uhakika nao wanafundisha uongo.
Mama mmoja hapo kijijini alikuwa na tatizo
la kutoka usaha mfululizo kwa zaidi ya mwaka mmoja,dada akamwambia mpigie ndg
kambarage akuombee,huku akiwa ametembea hospitali nyingi pamoja na kuombewa
katika madhehebu mbalimbali bila mafanikio, aliponipigia nikamwambia unaamini
?akasema ninaamini,nilikuwa ofisini,tukaomba kwa Bwana,naye Bwana akasikia
akamponya,nilipompigia jioni ya siku hiyo, alikuwa na furaha ya ajabu asiamini
kabisa kama shida yake imeisha,moto umeendelea hapo kijijini na familia ya
Branhamu inaongezeka.tunaomba maombi yenu ili tusonge mbele kumtafuta kondoo wa
mwisho kisha tuende kwa baba,AMEN
Bro.kambarage
TANZANIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni