Umishonari Zanzibar

Kwa miaka takribani miwili niliwahi kuongea na mchungaji KIMARO kwa ajili ya kwenda kumtembelea,kila tukiweka miadi  alikuwa anapoteza simu na nilikosa mawasiliano kwa mda mrefu,ikawa mwishoni mwa mwezi wa wa saba nilasikia sauti ya Bwana yenye nguvu sana kwamba nimpigie mchungaji Kimaro,.
        Nilipo mpigia akashangaa sana kumbe naye ananitafuta kwa mda mrefu,ndipo nikamwambia mchungaji   tungependa kuja kuwatembelea kwa wiki mbili zijazo,akasema haina shida karibuni sana,tukaomba kibali kwa Bwana, na akatupa tukafika salama sana siku ya tarehe   9/8/2013,tukaanza mkutano jioni hiyo ya ijumaa,na siku iliyofuata jumamosi  na tukamalizia siku ya jumapili tarehe 11/8/2013 ulikuwa ni mkutano wenye Baraka sana,na ambao ilikuwa ni ngumu sana kuagana,..
          Ilipofika siku ya jumatatu mchungaji akasema tukawatembelee baadhi ya ndugu na dada ambao wapo mashambani  tulienda na tukafika huko na kuwakuta ndugu na dada ambao ni wa Baraka sana,wanaishi katikakati ya waislam,.kama ujuavyo Zanzibar zaidi  95% ni waislamu tu,
    Tulipokuwa kule Mchungaji alituambia kuwa tuna paswa kuwa makini sana kwa sababu vile tulivyovaa tunajulikana kama ni wakristo na hivyo wako makini sana kuangalia tunfanya nini,kwa sababu baadhi ya ndugu walipigwa marufuku kushuhudaia huko na kuonekana huko.tulienda tukumkuta ndugu na dada JOHN huko shambani katika nyumba ndogo na za nyasi kama unavyoona kwenye picha hapo chini.walitukribisha kwa furaha sana moyoni lakini furaha yao ilizuiwa na mazingira kwani alituomba kuwa tusiombe kwa mda mrefu kwani tutakapoondoka tutamuachia matatizo makubwa nasi tulifanya hivyo ndani ya dakika kumi tuliwaaga hawa bi arusi wa thamani wa kristo.
   Baada ya hapo tulianza safari ya kumtembelea dada MONICA,tulimkuta yeye na binti yake mdogo wakiwa katika kibanda kikukuu cha nyasi lakini wakiwa wenye furaha sana,kama ujuavyo upendo wa kiungu ulioko katika familia ya Branham.Tulikaa hapo kwa dakika kama kumi tukamtia moyo sana na kwa kweli ilikuwa ngumu sana kuagana ndani ya dakika kumi wakati mnatamani kukaa zaidi ya siku mkiumega mkate wa Bwana.
   Tuianza safari ya kwenda mkoa mwingine tena shambani kumtembelea ndugu Herman na wengine huko,tulifika salama na tukakuta ndugu amewakusanya baadhi ya ndugu na dada,tukawa na ushirika wa neno kwa mda kama saa moja,na hawa watu masikini wa shambani, Bwana akafanya njia kwao wakaamini ujumbe wa nabii wetu,tukapanga kesho yake ya tarehe 12/8/2013 waje mjini tuwabatize baharini,ilipofika siku hiyo waliwaambia na wenzao ambao hawakuwepo siku ya tukio nao wakasema nasi tunaenda kubatiza,wakaja jumla yao nane tukawabatiza siku hiyo,ilikuwa ni furaha iliyoje hapo baharini? Bwana anajua.
  Huku zikiwa zimebaki kama dakika kumi ili boat iondoke kurudi Dar es Salaam,ambayo ndio tulikataa tiketi zetu,tulimuomba Bwana  kuwa afanye kama alivyofanya kwa nabii wetu kusimamisha ndege kwa ajili ya bibi arusi mmoja aliye kuwa wa thamani machoni pa Bwana, huku sisi tukiwa nao wanane.Bwana alijibu  tulikuta haijaondoka,tulipopanda tukakumbatiana kwa busu takatifu mimi na ndugu yangu wa thamani CHARLES,tukipongezana na huku abiria wakituangalia wasijuea furaha yetu inatoka wapi.
Baada ya hapo Bwana aliendelea kuwasha moto kwaani jumapili iliyofuata kanisa lilijaa na wengine wawili wakabatizwa na mchungaji amekuwa na huduma ya kuwatembelea mara kwa mara kuwatia moyo, na ili waje kanisani ina mlazimu kuwalipia nauli kwaani wengi wao ni masikini mno.PIA KUMEKUWA NA BAADHI YA WAAMINIO WA SIRI AMBAO WAMEBATIZWA LAKINI HAWAJAJITANGAZA WAZI KWANI WAKIFANYA HIVYO KUNA HATARI YA KUCHINJWA.
TUNAMUOMBA BWANA  ATUPE KIBALI CHA KUFANYA MKUTANO MKUBWA SANA ZANZIBAR MWEZI WA KUMI ILI BWANA AWEZE KUIBUA WENGINE HUKO KWAANI TUNAAMINI WAPO,TUNAOMBA MOMBI YENU,MUOMBEE MCHUNGAJI KIMARO NA FAMILIA YAKE, NI NDG WA BARAKA SANA WAMEJITOA KIKAMILIFU KUMTUMIKIA BWANA KATIKA MAZINGIRA HAYO MAGUMU.
  BROTHER KAMBARAGE

TANZANIA


Picha za matukio zanzibar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni